Ziara ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dodoma.

Posted on: 02.11.2026

Ziara ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dodoma.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg. Hassan Ali Haji amekutana na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Baraka Ildephonce Leonard katika ofisi za Bunge Dodoma kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kikazi baina ya taasisi mbili hizo za Kibunge.

Kukutana makatibu hao kunadhihirisha umuhimu wa kudumisha uhusiano wa ofisi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania hasa katika kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Katika mazungumzo yao pande zote mbili zimeonesha umuhimu wa kudumisha uhusiano wa karibu kwa kuimarisha na kuweka misingi imara ya mawasiliano na kujifunza mbinu bora za usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kibunge.

// //