Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 12 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 11.09.2023
Mkutano wa Kumi
na Mbili wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya
Jumatano tarehe 13 Septemba, 2023, saa 3:00 asubuhi.
A: SHUGHULI
ZA BARAZA:
Shughuli za Mkutano huo zitakuwa
kama ifuatavyo:-
1. Maswali na Majibu.
Afisi ya Baraza la Wawakilishi
imepokea na kuratibu maswali 116 kwa ajili ya Mkutano huu.
2. Ripoti za
Wizara zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu utekelezaji wa Maoni,
Ushauri na Mapendekezo ya Kamati za Kudumu za Baraza kwa mwaka 2022/2023.
3. Ripoti za Kamati ya Kuchunguza na
Kudhibiti Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti
Hesabu za Serikali za Mitaa na Mashirika (LAAC) za mwaka 2020/2021.
4. Taarifa ya Serikali Kuhusu Ripoti
ya Jitihada za Utekelezaji wa Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar mwaka
2022