Spika Zubeir aongoza Bonanza Arusha.

Posted on: 02.08.2026
Spika
Zubeir aongoza Bonanza Arusha.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid amesema mabonanza ya
michezo ni muhimu katika kujenga Taifa lenye afya, upendo na heshima katika
jamii.
Mhe. Zubeir ameyaeleza hayo wakati akifungua bonanza
lililowashirikisha Wajumbe wa Baraza hilo na Timu ya Arusha Wazee Sport Club
lililofanyika katika kiwanja cha Future Stars Academy jijini Arusha.
Amesema Bonanza hilo ni sehemu muhimu kwa Baraza la
Wawakilishi katika kulitumia kama chombo cha kuwaleta Pamoja viongozi na jamii
kwa lengo la kudumisha udugu kupitia michezo na kutoa msukumo kwa jamii kwa
lengo la kudumisha udugu kupitia michezo na kutoa msukumo kwa jamii katika
kuunga mkono michezo.
Washiriki wengine wa Bonanza hilo wamependekeza
Bonanza hilo liendelee kuwa kigezo muhimu cha kuunganisha Taifa na kukuza
utalii kupitia michezo ili jamii iwe na afya bora.
Bonanza hilo lilijumuisha mechi ya mpira wa miguu,
mpira wa pete, kuvuta Kamba, mchezo wa bao, mchezo wa viti (chair dancing), mbio
za magunia na marathon ya kilomita sita.