SPIKA ZUBEIR AWASISITIZA WANAFUNZI UMUHIMU WA ELIMU YA UONGOZI BORA.

Posted on: 19.06.2026

SPIKA ZUBEIR AWASISITIZA WANAFUNZI UMUHIMU WA ELIMU YA UONGOZI BORA.

Wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya  Olgun Boys  wamepata fursa ya  kutembelea na kukutana ana kwa ana na Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.

Katika mazungumzo mafupi na wanafunzi hao Mhe Spika amewasihi vijana hao kujitahidi katika masomo yao na kujenga tabia ya uongozi bora tangu wakiwa shuleni.

Baraza la Wawakilishi limekua ni sehemu ya programu za kuelimisha umma kuhusu  majukumu ya Baraza la Wawakilishi na ushiriki wa wananchi katika masuala ya uongozi.

//