Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 18 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 10.02.2025

Mkutano wa Kumi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 12 Februari, 2025, saa 3:00 asubuhi.

A: SHUGHULI ZA BARAZA

Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

1.   Maswali na Majibu.

Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 190 kwa ajili ya Mkutano huu.

 

2.   Miswada ya Sheria.

Miswada ya Sheria iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa mwezi Disemba, 2024 itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika Mkutano huu wa Kumi na Nane. 

 

Miswada yenyewe ni:-

(i)           Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma, Nam. 11 ya 2016 na Kutunga Sheria ya Ununuzi wa Umma na Kuweka Masharti Bora ya Kusimamia na Kudhibiti Ununuzi wa Umma na Mambo Mengine Yanayohusiana na HHHHHayo.

(ii)         Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Baraza la Udhibiti wa Mfumo wa Utoaji Leseni za Biashara, Nam. 13 ya 2013 na Kutunga Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Utoaji Leseni za Biashara Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na hayo.

3.   Uwasilishwaji wa Ripoti za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa Mwaka 2024/2025.

 

4.   Taarifa ya Serikali ya Mwelekeo wa Mpango wa Taifa 2025/2026.

//