Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 11 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 09.05.2023
Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 10 Mei, 2023, saa 3:00 asubuhi.
A: SHUGHULI ZA BARAZA
Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1. Maswali.
Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 246 kwa ajili ya Mkutano huu.
2. Majadiliano ya Bajeti
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
3. Miswada ya Sheria.
Miswada minne ya Sheria
itawasilishwa na kujadiliwa, Miswada yenyewe ni:-
i.
Mswada
wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)
ii.
Mswada
wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2023/2024.
iii. Mswada wa Kufuta Sheria ya Kuzuiya Rushwa na
Kuhujumu Uchumi Zanzibar Nam. 1 ya Mwaka 2012 na Kutunga Upya Sheria ya Kuzuia
Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
iv. Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Shirika la
Mawasiliano Zanzibar na Kuweka Masharti Yanayohusiana na Huduma ya Miundombinu
ya Tehama na Mambo Mengine Yanayohusiana na hayo.
4. Miswada Kusomwa mara ya Kwanza
5. Mengineyo kwa ruhusa ya Mwenyekiti