Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 14 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi
Posted on: 12.02.2024
Mkutano
wa Kumi na Nne wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza
siku ya Jumatano ya tarehe 14 Februari, 2024, saa 3:00 asubuhi.
A: SHUGHULI ZA BARAZA
Shughuli
za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:
1. Maswali.
Afisi
ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 181 kwa ajili ya Mkutano
huu.
2. Uwasilishwaji
wa Ripoti za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa Mwaka 2023/2024.
3. Miswada ya Sheria.
Miswada
miwili ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano kilichopita, itasomwa
kwa mara ya pili na kujadiliwa katika kikao hiki; miswada hiyo ni:-
i)
Mswada wa
Sheria ya Kufuta Sheria ya Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Nam. 12 ya 2019
na Kutunga Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar Kusimamia Huduma za
Serikali Mtandao Zanzibar na Mambo Mengine yanayohusiana na hayo.
ii)
Mswada wa Sheria
ya Kufuta Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar. Nam. 3 ya 2011 na
Kutunga Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar kwa
ajili ya Kutoa Msaada wa Kifedha wa Wanafunzi na Mambo Mengine yanayohusiana na
hayo.
4. Taarifa ya Wabunge watano (5) wanaoliwakilisha
Baraza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
5. Ripoti ya
Mapendekezo ya Muelekeo wa Mpango wa Taifa.
6. Ripoti ya
Utekelezaji wa Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamati ya Kuchunguza na
Kudhibiti Hesabu za Serikali (PAC) kwa mwaka 2020/2021.
7. Ripoti ya Mwaka ya Mamlaka ya Dawa
za Kulevya, Zanzibar 2022/2023.