Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 13 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi
Posted on: 27.11.2023
Mkutano
wa Kumi na Tatu wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza
siku ya Jumatano tarehe 29 Novemba, 2023, saa 3:00 asubuhi.
SHUGHULI ZA
BARAZA
Shughuli
za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1. Kiapo cha
Uaminifu cha Mjumbe.
Mwakilishi
Mteule wa Jimbo la Mtambwe Mhe. Mohamed Ali Suleiman ataapishwa kuwa Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi.
2. Maswali na
Majibu.
Afisi ya Baraza la Wawakilishi
imepokea na kuratibu maswali 88 kwa ajili ya Mkutano huu.
3.
Miswada ya Sheria.
Miswada ya Sheria iliyowasilishwa
na kusomwa kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa mwezi Septemba, 2023 itasomwa
kwa mara ya pili na kujadiliwa katika Mkutano huu wa Kumi na Tatu.
Miswada yenyewe ni:-
1.
Mswada
wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Kuanzisha Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali, Nam. 11 ya 2003 ya Kutunga Sheria ya Ukaguzi wa Umma na
Kuweka Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
2.
Mswada
wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Mahakama ya Kadhi Nam. 9 ya 2017 na Kutunga
Sheria ya Mahakama za Kadhi na Kuweka Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
3. Mswada wa Sheria ya Kuweka Masharti ya Utoaji
Leseni, Kudhibiti na Kusimamia Biashara ya Huduma Ndogo Ndogo za Fedha Kwa
Ajili ya Kudumisha Utulivu, Usalama na Ubora wa Huduma Ndogo Ndogo za Fedha na
Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
4. Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Mamlaka ya
Kukuza na Kulinda Uwekezaji Zanzibar, Nam. 14 ya 2018 na Kutunga Sheria ya
Uwekezaji Zanzibar na Kuweka Masharti Mengine Yanayohusiana na Hayo.
5. Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa
Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar na Kuweka Mambo Mengine Yanayohusiana
na Hayo.
6. Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Wakala wa Bohari Kuu
ya Dawa Zanzibar kwa ajili ya Ununuzi, Utengenezaji, Uhifadhi na Usambazaji wa
Dawa na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
4.
Taarifa ya Serikali kuhusu Ripoti ya Saba ya Utekelezaji wa kazi za Tume ya Maadili kwa mwaka 2022/2023