Spika awaapisha Wajumbe wawili wapya

Posted on: 16.09.2026

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid amewaapisha Wajumbe wapya wawili kufuatia uteuzi wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Septemba 14, 2026.

Wajumbe walioapishwa ni Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui na Mheshimiwa Omar Said Shaaban wote kutoka Chama cha ACT Wazalendo.

Kuapishwa kwa Wajumbe hao ni Hatua muhimu inayowapa nafasi ya kuanza kutekeleza majukumu yao rasmi ndani ya Baraza, ikiwemo kushiriki katika mijadala na shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo na masuala ya wananchi wa Zanzibzr.

Kuapishwa kwa Wajumbe hao kunakamilisha idadi ya Wajumbe 82 kwa mujibu wa kifungu cha 64 cha Katiba ya Zanzibar toleo la 2020.   

Idadi hiyo imetokana na Wajumbe 50 kutoka Majimboni, 20 nafasi maalum za Wanawake (Special seat), nafasi 10 za Uteuzi wa Mheshimiwa Rais, nafasi 1 ya Mwanasheria Mkuu na nafasi moja ni ya Mheshimiwa Spika.

Baraza la Wawakilishi linaendelea na Mkutano wake wa Nne wa Baraza la Kumi na Moja, ambo ulianza tarehe 9 Septemba 2026.

 

//