HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

BLW, Bunge la Iran kushirikina zaidi

Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa Iran zinakusudia kutanua wigo wa mashirikiano  katika masuala ya Kibunge ili kubadilishana uzowefu na  mbinu bora za kuendesha vyombo hivyo duniani.

Aidha mashirikiano hayo  yanalenga kutafuta mbinu muwafaka zaidi za kuwajengea uwezo wajumbe , pamoja na  ushiriki mpana zaidi  wa wananchi katika vyombo vyao vya uwakilishi na utungaji wa sheria.

Makubaliana hayo yamefikiwa leo hii wakati wa Mazungumzo ya pamoja kati ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid  na Msaidizi Balozi katika Ofisii ya Ubalozi wa Iran hapa nchini bwana Mohammad Dehghani .

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani nnje Kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Viongozi hao kwa pamoja wamesifu ushupavu mkubwa na kujiamini kwa   viongozi wa Jamhuri ya watu wa Iran,  suala ambalo linachangiwa na kuwa na bunge imara la nchi hiyo.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao pia wamekubaliana kuendelea kuenziwa kwa ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Iran hasa katika masuala ya utamaduni na biashara.

Katika hatua nyengine msaidizi Balozi huyo wa Ubalozi wa Iran hapa nchini kwa niaba ya Spika wa Bunge la Iran amemuwalika rasmi Mheshimiwa Zubeir kutembelea rasmi bunge la nchi hiyo mwezi ujao.


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events

Stay connected