HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Timu ya Wawakilishi yaichapa Bandari katika mchezo wa kumpongeza Dr. Mwinyi

Naibu Spika  wa  Baraza la Wawakilishi Mhe. Mgeni Hassan Juma amewasisitiza wanawake  kujiamini na kushiriki katika  michezo mbali mbali kwani  ni fursa ya kujijenga  kiafya   na  kupata  ajira.

 

Akizungumza  katika kiwanja cha Gymkana wakati akifungua mchezo wa kirafiki wa kumpongeza rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kuingia madarakani uliozikutanisha timu ya netball za  Baraza la Wawakilishi dhidi ya timu ya bandari.

 

Amesema serikali ya awamu ya nane imedhamiria kulea, kukuza na kuendeleza vipaji vya  wana  michezo kwa kuandaa miundo mbinu rafiki ya michezo.


Katika mchezo huo timu ya baraza la wawakilishi iliovalia nyeupe jezi imefanikiwa kuifunga timu ya bandari kwa magoli 45 kwa 44   na   manahodha wa timu zote  wakauelezea  mchez  huo   kuwa   uliojaa   ufundi   na  ni  muhimu  katika  hatua  ya  kumpongeza   rais  wa    zanzibar.


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events