HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Taarifa ya shughuli za Mkutano wa Nne wa Baraza la Kumi la Wawakilishi


Mkutano wa Nne wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 08 Septemba, 2021, saa 3:00 asubuhi. Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo,

1. Maswali na Majibu.

Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 150 kwa ajili ya Mkutano huu. Hata hivyo, maswali 115 ndiyo yatakayopata nafasi ya kujibiwa na maswali 35 yatabakia mpaka kikao kijacho.

2. Miswada ya Sheria.

Miswada ya Sheria iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa mwezi Mei, 2021 itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika Mkutano huu wa Nne. Miswada yenyewe ni:-

i) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Ofisi ya Msajili wa Hazina na Usimamizi wa Mali za Umma na Mambo mengine yanayohusiana na hayo.

ii) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, na kuweka usimamizi mzuri wa shughuli za Kiislam Zanzibar na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

iii) Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali Mbali na kuweka masharti bora ndani yake.

3. Taarifa ya Serikali kuhusu mtumishi wa Serikali kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia Kitengo cha Benki ya Damu.

4. Taarifa ya Serikali kuhusu suala la ukodishwaji wa nyumba inayotumika kwa ajili ya vipimo vya Covid 19 Mazizini.

5. Taarifa ya Kamati ya Maadili na Kinga za Wajumbe kuhusu Malalamiko kutoka kwa Dkt. Hassan Rashid Ali dhidi ya Mhe. Ali Suleiman Ameir

(Raya Issa Msellem)
KATIBU
BARAZA LA WAWAKILISHI
ZANZIBAR.
Tarehe 06 Septemba, 2021


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events