HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Bwana Jassen Al- Najem amefanya ziara ya kikazi katika jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Chukwani mjini Zanzibar na  kukutana na Spika wa Baraza hilo Mheshimwa Zuberi  Ali Maulid ambae amesema kuwa Zanzibar inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya Kuwait kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na Zanzibar.

Mheshimiwa Zubeir amesema kuwa Zanzibar inafarijika na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Kuwait kupitria mfuko wake wa Kuwait Fund for Arab Economic Development ambao umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili nchi yetu katika sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya afya na elimu.

Aidha, Mheshimiwa Spika amesema kuwa atazishauri Kamati za kisekta za Baraza la Wawakilishi kuifuatilia kwa kina miradi mbali mbali inayofadhiliwa na wafadhili wa nje ikiwemo miradi inayofadhiliwa na Kuwait Fund for Arab Economic Development ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa kwa lengo la kuwanufaisha na kuwasaidia wananchi wetu.

Akitoa msisitizo katika kikao hicho, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Bwana Jassen Al- Najem amesema kuwa ni vyema kwa Tanzania na Zanzibar kuhakikisha kuwa inafuatilia miradi hiyo na kuiendeleza kwa mujibu wa makubaliano ya liyofikiwa ili faida iweze kuaptikana pamoja na kufungua milango ya misaada zaidia katika sekta mbali mbali.

Bwana Jassen amesemakuwa ni vyema kwa Zanzibar na Kuwait kuendeleza uhusiano wa kihistoria uliojenga tokea enzi za mababu ili historia ya nchi mbili huizi isiweze kupotea. Ameshauri kuanzishwa kwa utaratibu wa kujifunza kwa kubadilishana mawazo baina ya maafisa wa Serikali na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili lengo la kusaidiana liweze kutimia.

Katika kikao hicho, viongozi hao wawili wamekubaliana kushirkiana katika kazi zao kwa lengo la kuimarisha uhusiano baiana ya nchi zao ili wananchi waweze kunufaika na miradi mbali mbali itakayoanzishwa kupitia taasisi zao.

 

 


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events

Stay connected