Katibu wa BLW Ndg. Hassan Ali Haji akutana na VP1 na VP2.

Posted on: 20.10.2026
Katibu wa BLW Ndg. Hassan Ali Haji akutana
na VP1 na VP2.
Katibu wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg. Hassan Ali Haji amekutana na Makamu wa
Kwanza Mhe. Masoud Othman Masoud na Makamu wa Pili Mhe. Hemed Suleiman Abdullah
kwa nyakati tofauti.
Katibu
Hassan amekutana na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Masoud Othman Masoud katika Ofisi
ya Makamu wa Kwanza iliopo Migombani Wilaya ya Mjini Magharib Unguja.
Mapema Katibu
Hassan amekutana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika
Ofisi ya Makamu wa Pili Vuga Wilaya ya Mjini Unguja.
Lengo la
kukutana nao ni kujitambulisha baada ya Katibu Hassan kuteuliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Septemba
14, 2026 kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi.