Kamati ya Kanuni ya BLW yahimiza kufuata taratibu za Mikopo kwa ZHESLB.

Posted on: 20.10.2026

Wajumbe wa Kamati ya Kanuni na Sheria ndogondogo ya Baraza la Wawakilishi wameihimiza Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Zanzibar ( ZHESLB) kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa mikopo wa elimu ya juu na kuhakikisha taratibu za mikopo zinafuatwa.

Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Hudhaima Mbarak Tahir wamesema hayo baada ya kupitia Kanuni za jumla za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Zanzibar   na kusisitiza taratibu na utekelezaji wa urejeshaji mikopo ya elimu ya juu haziwi kikwazo kwa wanufaika.

Wameeleza kuwa endapo taratibu zitafuatwa vizuri zitawasidia wanufaika kukidhi mahitaji yao ya msingi na kujiimarisha kiuchumi.

Kwa upande wao wadau wa Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar wameiomba Bodi hiyo kuboresha na kuimarisha mifumo ya urejeshaji wa mikopo hiyo na kuhakikisha taratibu haziwabani wanufaika wa mikopo hiyo hususan wanapokuwa katika hatua za kujenga maisha yao baada ya kuhitimu masomo.

// //