BARAZA LA WAWAKILISHI SPORT CLUB YATOKA SARE YA 1-1 NA MADIWANI WA MAGHARIBI “B”.

Posted on: 19.05.2026
Timu ya mpira wa miguu
ya Baraza la Wawakilishi Sport Club imefanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 na Timu
ya Madiwani wa Wilaya ya Magharibi “B” uliochezwa katika Uwanja wa Kitogani.
Katika mchezo huo wa
kirafiki ,Timu ya Baraza la Wawakilishi Sport Club iolionesha kujipanga vyema
kutokana na kuonesha umoja wa hali ya juu katika kuumiliki mpira na kutafuta
nafasi za kutoka katika kuzishambulia nyavu za Timu ya Madiwani.
Goli la Timu ya Baraza
la Wawakilishi lilifungwa na Mhesimiwa Ali Abdulghulam Hussein ambae pia ni Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo baada ya kupokea pasi safi kutoka
kwa Mheshimiwa Mmanga Mohammed Hamed (Jimbo la Tumbe).
Mwenyekiti wa Baraza la
Wawakilishi Sport Club Mhe. Mahfoudh Abdalla Mohammed amesema ameridhishwa na kiwango
kikubwa walichokionesha wachezaji wake kwa vile ni mechi yao ya Kwanza tangu
kuanza kwa Baraza la 11 la Baraza la Wawakilishi.
Hata hivyo Mhe.
Mahfoudh amewahimiwa wachezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Sport Club
kuendelea na mazoezi ili kuwa na afya njema pamoja na kuendelea kufanya vizuri
zaidi katika mechi zijazo.
Kepteni wa Timu hiyo
Mhe. Khamis Mohammed Amrani (Jimbo la Mkoani) amesema lengo la Timu ya Baraza
la Wawakilishi Sport Club imeamua kucheza mechi hiyo ili kujenga mahusiano
mazuri na ukaribu zaidi na Wawakilishi katika sekta mbali mbali ikiwemo
michezo.
Mgeni rasmi katika
mchezo huo alikuwa ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Mwanaasha
Khamis Juma.