DKT. JUMA KUWASILIHA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Posted on: 15.06.2026
DKT. JUMA KUWASILIHA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Trilion 8.5 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Amesema katika Bajeti hiyo Serikali imekusudia kuendelea kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kwa ufanisi na tija kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.
Aidha alifafanua kuwa, katika Bajeti hiyo imehusisha kiwango cha mishahara mipya ya wafanyakazi itakayoanza rasmi Oktoba 2026 badala ya Januari 2027.
"Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu wa kuendelea kuhamasisha ari ya utendaji, kuongeza tija katika utumishi wa umma na kuboresha hali ya maisha ya watumishi.Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametuelekeza kuwa marekebisho ya mishahara ya watumishi wote kwa mujibu wa muundo wa utumishi (scheme of services) yaanze kutekelezwa mara tu baada ya kukamilika Robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2026/2027. Kwa mantiki hiyo, Mishahara mipya kwa watumishi wote itaanza kulipwa mwezi wa Oktoba 2026, badala ya ya Robo ya Tatu inayoanzia Januari 2027 iliyokuwa imepangwa awali." alifafanua
Waziri wa fedha pia alitaja vipaumbele vya serikali katika kutekeleza bajeti hiyo ikiwemo kuanzia soko la hisa la Zanzibar, kuimarisha upatikanaji wa mitaji na huduma za kifedha pamoja na kuongeza kasi ya usimamizi wa matumizi wa mifumo ya kielektronik katika ukusanyaji wa mapato.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wataanza kuichangia Hotuba hiyo ya Bajeti ya Serikali kunzia tarehe 15 Juni 2026.