Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho (kati) akisaini hati ya kiapo cha uaminifu baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Said Hassan Said (kushoto) katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa kumi na Saba wa Baraza hilo.

 

 

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakisoma Dua ya Baraza kwa siku ya kwanza kufuatia kuanza kwa Mkutano wa Kumi na Saba wa Baraza la Wawakilishi.

 

 

 

 

 

Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi na Wadau wa Wizara husika zinazosimamiwa na Kamati hiyo, wakiwa katika Kikao cha Kamati cha kujadili Mswada wa Sheria ya Shirika la Nyumba la Zanzibar ya mwaka 2014.

 

 

Washiriki wa mkutano wa tatuwa Bunge la Vijana la Nchi Wanachama wa Jumuia ya Madola kanda ya Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Zambia Mhe. Dkt Matibini mara baada ya ufunguzi rasmi wa Bunge Hilo. Mkutano huo unafanyika Nchini Zambia Tarehe 24 hadi 28 Agosti 2014.

 

 

 

 

 

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Mwanakwerekwe Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Namba 2 ya Bunge Maalum la Katiba akitoa maelezo ya Maendeleo ya Kamati yake kwa waandishi wa Habari. Bunge Maalum la Katiba linaendelea na Shughuli zake Mjini Dodoma ambapo kwa sasa Kamati mbali mbali zinaendelea kujadili Sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba.

 

 

Search the Site
Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati kuhusiana na mswada wa kufuta sheria ya wauguzi na wakunga Click to Read

Taarifa ya Spika katika Mkutano wa Kumi na Saba wa Baraza la Nane la Wawakilishi Click to Read

Orodha ya shughuli za leo, Tarehe 22 Oktoba 2014 Download

New Bills, 2014 Click to Read

Mkutano wa Kumi na Saba wa Baraza la Nane la Wawakilishi

Mkutano wa Kumi na Saba wa Baraza la Nane la Wawakilishi unatarajiwa kuanza kesho Jumatano Tarehe 22 Oktoba, 2014 saa 3.00 kamili Asubuhi. Akizungumza na Waandishii wa Habari katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo …....
Read more »


Wadau watoa mapendekezo yao juu ya Miswada itakayojadiliwa na Baraza katika mkutano wa kumi na saba.

Baraza la Wawakilishi Zanzibar linatarajia kuanza Mkutano wake wa Kumi na Saba kuanzia siku ya Jumatano tarehe 22/10/2014. Mkutano ambao utakua wa muda wa wiki mbili , unategemea. …....
Read more »


Taarifa ya kurejea kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Baada ya kumaliza mchakato wa kupitia Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kutunga Katiba inayopendekezwa, uliokamilika siku ya tarehe 2/10/2014 na kukabidhiwa kwa Rais. …....
Read more »


Mjumbe wa BLW aapishwa kuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba

  Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Makunduchi Mheshimiwa Haroun Ali ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba.
Mhe Haroun aliapishwa Agosti 5, mwaka huu na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta, pamoja na wenzake wawili ili kuungana na Wajumbe wenzao katika shughuli za utungaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazoendelea katika awamu yake ya pili Mjini Dodoma.


MEMBERS OF THE HOUSE

Questions
Supplementary Questions
Contributions
All members

Search House Members

Enter Name or Constituent